Arsenal inamfuatilia nyota wa Inter Milan raia wa Denmark Patrick Olsen kuangalia uwezekano wa kumnyakua dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi Januari kwa mujibu wa vyanzi vya Italia. (Talksport)

Mesh Mushobozi
Beki wa Atletico Madrid Juanfran ameitosa Arsenal uhamisho wa kipindi cha majira ya joto - ingawa Arsenal iliahidi kumlipa mara nne ya mshahara anaoupata Madrid. (AS)
Samuel Eto'o amefunguka kuwa alibakisha masaa machache kusaini mkataba na Arsenal mwaka 2000, kabla hajabadili uamuzi wake na kujiunga na Mallorca. (The Sun)
Chelsea inatarajia kumleta beki wa Sheffield United Harry Maguire dirisha dogo la uhamisho la Januari - ili kurithi nafasi ya John Terry'. (Metro)
Manchester United itajaribu tena kumsajili nyota wa Athletic Bilbao, Ander Herrera mwezi Junuari baada ya jitihada za kumsajili kipindi cha majira ya joto kugonga mwamba. (Daily Star)
Manchester United inajipanga pia kumsajili kiungo wa Barcelona aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Alex Song. (Daily Express)
Joleon Lescott amejipatia nafasi kikosi cha kwanza Manchester City lakini haiwezi kumzuia kuondoka klaabuni hapo Januari kwasababu Everton na Aston Villa zinamnyemelea. (Daily Mail)
Shabaha ya Arsenal, Ilkay Gundogan amekataa kuondoka Borussia Dortmund kwasababu yuko kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Ujerumani, Bundesliga kuona uwezekano wa kuongeza mkataba wake. (Daily Star).



0 comments:
Chapisha Maoni