Mchezo wa Ligi Kuu Bara katika ya Yanga na Mbeya City jana uliingiza kiasi cha Sh Milioni 100.
Watu 20,000 waliingia kwenye Uwanja wa Sokoine katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya mabao 1-1.
Kati ya hizo, Sh. Milioni 18 ni makato ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), gharama za tiketi Milioni 37, ghrama za Uwanja Milioni 6, MREFA wamepata Milioni 2.5, TFF Milioni 3.5, Kamati ya Ligi Milioni 7, na kila timu imepata Sh. Milioni 23.6.
Watazamaji 16,507 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 15 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,018,077.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,503,728.81.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,704,107.18, tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 7,022,464.31, Kamati ya Ligi sh. 7,022,464.31, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,511,232.15 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,730,958.34.




0 comments:
Chapisha Maoni