The reliable source of sport news

Jumapili, Novemba 10, 2013

HAUZWI MTU HAPA, MBEYA CITY

10.11.13 By Unknown No comments

KOCHA wa Mbeya City, Juma
Mwambusi ameonya kwamba hataki
kuona timu yoyote ikisogelea
wachezaji wake wakati huu wa
mapumziko na akasisitiza kwamba
hawauzwi “Not for sale” wala hayuko
tayari kufanya makubaliano yoyote.
Kocha huyo aliliambia Mwanaspoti
kuwa hatakibadili kikosi hicho na
hataafiki wachezaji kuuzwa kwani
anataka kuendelea nao kwavile tayari
wana msingi mzuri mpaka sasa na
wameonyesha nia ya kupiga hatua.
“Kama ni uamuzi wangu, sitamuachia
mchezaji yeyote kuchukuliwa na timu
nyingine, labda uongozi kama
utaamua. Nataka kuona wachezaji
wangu wakiwa wale wale kwenye
mzunguko wa pili kwani wamezoeana
na wanajua jinsi wanavyocheza,”
alisema Mwambusi akidai kwamba
anatarajia baadhi ya timu zenye
fedha zitaanza kuzengea wachezaji
wake kama kawaida yao.
Mwambusi amekiongoza vyema kikosi
cha Mbeya City kwenye mzunguko wa
kwanza wa ligi na haijapoteza
mchezo wowote huku ikishikilia
nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na
Azam.
Mbeya City ni kati ya timu tishio
katika Ligi Kuu Bara ambayo juzi
Alhamisi ilifikia tamati kwa
mzunguko wa kwanza na kwa sasa
timu ziko katika mapumziko hadi
Januari mwakani.

Kwa hisani ya Mwanasport.

0 comments:

Chapisha Maoni