YANGA na Azam kama zinamtaka straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ni fedha yao tu, lakini kuna sharti lazima walifanye.
Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limetoa masharti
na muongozo wa klabu zinazomtamani mchezaji huyo aliyesitisha mkataba na
Etoile du Sahel ya Tunisia.
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba
aliiambia Mwanaspoti kuwa: “Hakuna kinachoizuia klabu kutaka kumsajili
Okwi, cha muhimu wanatakiwa kuongea na Etoile du Sahel ya Tunisia,
wakimalizana nao basi watamchukua, hivyo ni ruksa cha muhimu ni kufuata
sheria na haki.”
Okwi ameidhinishwa na Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa) kuichezea SC Villa ya Uganda kwa muda wa miezi sita
huku sakata lake la Etoile likifanyiwa ufumbuzi.
Mchezaji huyo anaidai Etoile malimbikizo ya
mishahara pamoja na dau lake la usajili huku Simba iliyomuuza kwa
Waarabu hao nayo ikidai dau lake Sh 480 milioni.
Suala hilo lipo Fifa na Kawemba amewahakikishia Simba kwamba wasiwe na wasiwasi watapata haki yao.
Source: Mwanasport
Source: Mwanasport




0 comments:
Chapisha Maoni