Beki wa Chelsea David Luiz ameripotiwa kuwa hitaji namba moja la Barcelona baada ya kushindwa kumpata nyota wa Paris Saint-Germain Thiago Silva.
Wababe hao wa Katalan wamekuwa wakimhitaji Thiago Silva kwa muda mrefu lakini mchezaji huyo alionyesha kuvutiwa kubaki kwenye klabu hiyo ya Ufaransa inayoshiriki Ligue 1. Inaonekana sasa Blaugrana imehamishia majeshi kwa mbrazili mwenzake anayekipiga klabu ya Chelsea David Luiz ambaye ameshaanza mazoezi kwa ajili ya kuanza msimu chini ya kocha mpya Jose Mourinho. Wakala wa mchezaji huyo, Giuliano Bertolucci, imeripotiwa kuwa ameshafanya mazungumzo ya awali na Mkurugenzi wa Barca, Andoni Zubizarreta. Bayern Munich nayo imeonesha nia ya kumhitaji nyota huyo jambo linaloashiria ugumu kwa Barca kuipata saini ya Luiz endapo Chelsea itakuwa tayari kumruhusu kuondoka London.




0 comments:
Chapisha Maoni