Tangu Jose Mourinho
aondoke Real Madrid klabu imetumia pauni milioni 34 kumpata Kiungo wa Real
Sociedad Asier Illarramendi jambo linaloonekana kumshusha mchezaji wa kimataifa
wa Ujerumani Sami Kedira kiwango.
Na Kedira ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao hawajawahi kupishana na Mourinho katika msimu wake wa mwisho La Liga alipokuwa na timu hiyo, jambo ambalo litampa nafasi nzuri ya kumfuata kocha huyo Chelsea.

Mourinho amesema
anataka kiungo anayeweza kumiliki mpira na Khedira anaonekana kuwa na sifa hizo
zaidi ya nyota wa Roma Danele De Rossi kwa mujibu wa The Mirror.
Khedira, 26, anaweza
kuigharimu Chelsea wastani wa pauni milioni 20 hivi, pamoja na ujira wa pauni
milioni 4 kwa mwaka. Kiungo huyo wa zamani wa Stuttgart ameichezea Real Madrid
mara 103 katika michuano yote tangu alipoanza kucheza La Liga mwaka 2010 na
amefunga magoli saba.

0 comments:
Chapisha Maoni