Manchester United watageuzia macho yao kwa nyota wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger – iwapo ofa yao ya tatu itakataliwa na Barcelona kwa ajili ya Cesc Fabregas wiki hii.
Mabingwa hao wa Ligi ya Uingereza wanatambua tetesi toka Ujerumani kwamba Schweinsteiger si chaguo la Pep Guardiola katika kikosi chake hicho cha Bavaria.
Na Manchester United inatafuta kwa hali na mali, jambo linaloonesha kwamba kiungo huyo wa Ujerumani anaweza kuwa mbadala endapo dili la Fabregas litakwama.
Inaaminika kwamba Fabregas mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari na anataka kwenda Old Trafford lakini timu yake haiko tayari kumwachilia.
Lakini, kama Barca ikiendelea kusisitiza kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal hauzwi, United italazimika kutazama namna nyingine mapema.
Na Real Madrid nayo inaendelea kusisitiza kwamba hawako tayari kusikiliza ama kupokea ofa yoyote inayomuhusu Luka Modric.
Habari kwamba Schweinsteiger atahitaji kufanya kazi ya ziada kumshawishi Pep Guardiola kumpa nafasi kikosi cha kwanza Bayern zinaipa Manchester United fununu kwamba mchezaji huyo ananunulika.
Guardiola amerithi timu hiyo inayoshikilia taji la klabu bingwa Ulaya na ubingwa wa Bundesliga lakini ameweka wazi kwamba hataki kutumia mfumo unaohitaji viungo wakabaji wawili.
-855075.jpg)




0 comments:
Chapisha Maoni